KOSSAM, Ni jina lenye maana ya utawala, uongozi na umiliki kwenye misingi ya familia/ Ukoo wa MWAKOSSAM. Ni jina analopewa Mtoto au Mzaliwa wa kwanza wa kiume ndani ya ukoo wa MWAKOSSAM (hutumiwa na watoto wa kiume pindi wapatapo watoto wao wa kwanza wa jinsia ya kiume). Wazaliwa wa kwanza wa kiume hupewa jina hili wakitazamiwa kuwa wao ndiyo WASIMAMIZI wa Mali na miradi ya familia/ukoo wakifuatiwa na ndugu wengine ndani ya ukoo wa MWAKOSSAM. Watoto wakike ndani ya Ukoo wa MWAKOSSAM hawaruhusiwi kutumia jina la KOSSAM kuwapa watoto watakao wapata, maana wao wataolewa na kuzaa na watu kutoka koo zingine ambao damu wala vinasaba vyao havitaruhusiwa kurithi na kumiliki Mali ndani ya Ukoo wa MWAKOSSAM.