Deusdedith Binamungu Severian alizaliwa 5 Agosti 1983 katika Kitongoji cha Bikiri Kijiji cha Katembe Kata ya Kituntu Wilaya ya Karagwe Mkoani Kagera nchini Tanzania. Elimu: Mwaka 1993 alijiunga katika Shule ya Msingi Katembe na kuhitimu Mwaka 1999 ambapo alifaulu Mtihani wa Taifa na kuchaguliwa kujiunga na masomo ya sekondari kuanzia mwaka 2000 na kuhitimu Kidato cha Nne mwaka 2003 katika Shule ya Sekondari Rwambaizi.
Baadaye alichaguliwa kuendelea na masomo ya Kidato cha Tano na Sita katika Shule ya Sekondari Chato iliyopo Wilayani Chato Mkoani Geita. Alijiunga na Shule hii mwaka 2004 na kuhitimu mwaka 2006.
Mwaka 2007 alijiunga na masomo ya Shahada ya Kwanza (B.A.in Geography and Environmental Studies) katika Chuo Kikuu cha Dar es Salaam, Tanzania na kuhitimu mwaka 2010.