Harold Mrosso ni Baba wa familia,mume kwa mwanamke mrembo, msomi na mwenye staha Eva saimon na wanaishi kwa upendo na Mtoto wao kipenzi Dawson junior pia ni mfugaji maarufu wa mbwa wa ulinzi na mmiliki mwenza wa duka la za binadamu (HED DUKA LA DAWA NA VIPODOZI) linapatikana kasulu mjini mkoani kigoma.
Alizaliwa mbeya (Meta Referral Hospital) na marehemu mama yake mpendwa Mwl. Kissah Mwakamyanda huku baba yake kipenzi Dr. D. E. Mrosso akiwa Mganga mkuu wa hospital hiyo kubwa ya mama na mtoto mkoani Mbeya.
Ni mzaliwa wa mwisho kati ya watoto watatu wa Marehemu mama yake wengine ni marehemu kaka yake Dr. Emmanuel Mwakamyanda na dada yake mpendwa Faraja Mwakamyanda mwenye makazi yake Dar-es-salaam, Tanzania.
Harold Mrosso