Mtoto wa Kwanza Katika Familia ya Watoto amejaaliwa kusoma mpaka kidato cha nne na baadae kwenda kusomea elimu ya Utangazaji na Uandishi wa Habari, Kwa Bahati mbaya hakujaaliwa kumaliza Taaluma hiyo kutokana na ukosefu aa pesa ya kumalizia Masomo yake hayo aliyokuwa akisomea kwa ngazi ya cheti, Baadae akaamua kuingia mtaani kufanyia kazi kile alichojifunza shule 2017 alienda Dar Es Salaam kwa lengo la kutafuta kazi ya Utangazaji lakini kwa bahati mbaya hakufanikiwa kupata Kazi na kurejea moshi na kuanza kufanya kazi kwenye Radio ya Dini kwa muda wa Miaka miwili

AMEWAHI KUFANYA KAZI KWENYE RADIO NA TV MBALI MBALI NA MASHIRIKA YA KIBINAFSI YA KUSAIDIA WATU WENYE UHITAJI. . Kwasasa Said Mbegu anatambulika kama mmiliki wa You Tube Channel Inayofanya Vizuri inayotambulika kwajina La @MOtownTV