Charles Sylvester Turuka,Maarufu kama Mc Turuka,AlizaliwaTarehe 05/04/1992. katika familia ya Mzee. Sylvester Turuka na Bi. Regina Makenge Akiwa ni mtoto wa 10 kati ya watoto 12 wa Familia hiyo.
Elimu yake ya msingi aliipata Shule ya Msingi Mugumu mwaka 2001 na kuhitimu mwaka 2008 na Kisha Kujiunga na Elimu ya Sekondari mwaka 2009,katika shule ya Sekondari Mugumu iliyoomo Serengeti Mkoani Mara.
Baada ya Hapo alianza Kujiajiri na Baadaye akianza Tasnia hii ya Uneni akisimama Jukwaani Kwa Mara ya kwanza kama Mshereheshai (Mc) mwaka 2017 huko Sirari
Mpaka sasa Mc Charles Turuka ni Mshereheshaji machachali sana anayekuja Kwa Kasi na anayefanga kazi nzuri akitokea Sirari Mkoani Mara..