GWARA Gwara ni jina lenye asili ya kitanzania. Limechukua nafasi katika jamii kubwa ya kitanzania huku watumiaji wake wakiwa ni wachache.

Miongoni mwa jamii ya watu wanaotumia jina hili ni wenyeji wa mji wa Tanga.

Katika Jiji Hilo kubwa nchini Tanzania. Jina GWARA ni maarufu sana katika kijiji Cha kasanga kata ya mtimbwani wilaya ya mkinga. Vilevile Katika vijiji jirani vya kwale na kizingani.

Umaarufu wa jina hili katika maeneo hayo unaakisiwa kupatikana mwanzoni mwa mwaka 1940.kwa familia ya watu wenye asili ya bara la Asia nchini Iran. Waliohamia katika Jiji Hilo la Tanga mwishoni mwa mwaka 1890.kizazi hiki Cha wageni Hawa wenye asili ya irani inafahamika kilianzishwa na mgeni kutoka katika nchi hiyo ya Iran katika kabila la Kurds. Aliyefanya safari zake za kibiashara katika mji huo. Alifahamika Kwa jina la Ali Khan.

Kizazi hiki Cha Kurds katika mji huo kilipoteza asili yake, baada ya muanzilishi wake Ali Khan kuondoka na kuacha mke na mtoto mmoja wa kiume wa jamii ya watu Hawa wa Kijiji Cha kasanga. Aliyepewa jina la Mohammed Ali Khan. Ambapo kupitia yeye bwana Mohammed Ali Khan ndipo kilipopatikana kizazi Cha Ali (gwara) Mohammed, mwinyijuma bin Mohammed Ali Khan.

Mnamo mwanzo mwa Karne ya 19.kizazi hiki Cha gwara katika Jiji la Tanga kilipatikana. Kwa kuzaliwa muasisi wake Mzee gwara (Ali Mohammed, mwinyijuma bin Mohammed Ali Khan).

Ali Mohammed (gwara) alioa katika kitongoji Cha birikau Kijiji Cha michungwani gombani, chakechake Pemba. Familia ya athumani fakhi. Na kuasili kizazi Cha watoto nane. Wakiwemo Aisha Ali Mohammed, Ali Ali Mohammed, mwantime Ali Mohammed, Mohammed Ali Mohammed, athumani Ali Mohammed, suleimani Ali Mohammed, swaleh Ali Mohammed na Fatma Ali Mohammed.

Ali Ali (gwara) Mohammed na Mohammed Ali (gwara) Mohammed baadaye walihamia wilaya ya mpwapwa jijini Dodoma. Waliobaki waliishi katika Jiji la Tanga. Wakijishughulisha na biashara na uvuvi Kwa kiasi kikubwa. Pamoja na kuhusika katika ujenzi wa taifa Kwa nafasi mbalimbali za utumishi wa umma.