Kalamu dumu daima. Ni kalamu yenye wino wa maneno ya busara, heshima na mafunzo muhimu kwa kila msomaji. Maneno haya ni mfumo wa mashairi,nakala na riwaya za kuvutia ndani ya ulimwengu wa fasihi andishi. Dira ya kazi hii ni kuangaza taaluma ya lugha adhimu ya Kiswahili. Ungana nami; Hamdan Mohamed, Mwandazi wa safari hii ya kioo cha ulimwengu wa lugha.
Kalamu dumu daima, milele bila kuvuma Andika andiko jema, mbele ya Mola Karima Utunge tungo adhima , sifa ziwe za heshima Nakili maneno mema , maneno yenye hekima
Kalamu toa kalima, kalima iliyo wima Mimina wino mzima, kwa heshima na taadhima Maneno mbele na nyuma, yanataka taaluma .....................
Dhamira ya kalamu hii ni kuenea kuanzia mashinani hadi vileleni vya uandishi bora.